Mabasi mapya ya mradi wa mwendokasi hatimaye yamewasili kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Mbagala Rangi Tatu! Usiku wa Agosti 29, mabasi hayo yalianza kuingizwa kituoni yakitokea Bandari ya Dar es Salaam.
Hii ni hatua kubwa kwani mradi huu unatarajiwa kubadilisha kabisa hali ya usafiri jijini. Katika awamu ya kwanza, mabasi 255 yataanza kutoa huduma. Lengo ni kufikisha jumla ya mabasi 755, ambayo yanatarajiwa kusafirisha hadi abiria 350,000 kila siku.
Huduma hiyo itaanza rasmi Jumatatu, Septemba Mosi, ambapo mabasi yataanza safari kutoka Mbagala kwenda Gerezani na Kivukoni.